Mafunzo ya Udereva wa Kujihami kwa madereva wa kampuni ya TBL Mbeya


Tarehe 16/06/2019 Kampuni ya Mbenapa Holdings (T) Ltd ilitoa mafunzo ya Udereva wa Kujihami katika Kampuni ya kutengeneza vinywaji ya TBL mkoani Mbeya. Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea madereva ujuzi na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakuta madereva wa magari makubwa yanayosafiri masafa marefu. Mafunzo haya yamewawezesha madereva kuweza kuendesha Magari yao kwa usalama na weledi wa hali ya juu na kuweza kuepusha ajali ambazo aidha wangesababisha au kusababishiwa na watumiaji wengine wa barabara

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *